23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Uturuki yatuma ujumbe wa pole kwa Indonesia

Instanbul, Uturuki

Uturuki imechapisha ujumbe wa rambirambi kuwafariji wananchi na serikali ya Indonesia kufuatia vifo vilivyosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje, iliandikwa,

“Tumepokea kwa masikitiko taarifa za kutokea kwa tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha 6.2 katika mji wa Majene, Magharibi mwa Sulawesi nchini Indonesia, na kusababisha vifo vya watu wengi na majeruhi,”

Taarifa iliambatana na ujumbe wa pole kwa serikali, wananchi wa Indonesia, ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliopoteza maisha kwa kuwaombea Mwenyezi Mungu awarehemu, pamoja na kuwatakia afueni ya haraka majeruhi wote wa maafa hayo.  

Mwenyekiti wa Wakala wa Maafa katika kanda ya Sulawesi Magharibi, Darno Majid, alitangaza idadi ya vifo iliongezeka hadi 35 hadi kufikia sasa kwa mujibu wa taarifa walizopokea awali, baada ya tetemeko la ardhi kutokea mjini Majene.

Tetemeko hilo la ardhi limesababisha watu 637 kujeruhiwa, na zaidi ya wengine elfu 15 kuhamishwa makaazi yao hadi sasa. Timu ya utafutaji na uokoaji bado inaendeleza juhudi zake katika mkoa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles