27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Uturuki waonesha nia kuleta madaktari bingwa JKCI

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

UBALOZI wa Uturuki nchini umeonesha nia ya kuanza kuleta kwa mara ya kwanza madaktari bingwa wa moyo kuja kushirikiana na wenzao katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Yalielezwa hayo hospitalini hapo jana na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi wakati wa ziara fupi ya ujumbe uliotumwa na ubalozi huo, ulioongozwa na Profesa Serdar Ener wa Hospitali ya Medicana iliyopo Bursa nchini Uturuki.

“Tulianza mazungumzo na ubalozi kabla hata taasisi hii kuanza rasmi, sasa ndiyo tumeanza utekelezaji, tumelenga mambo makuu mawili.

“Moja ni ushirikiano ambapo wao (Uturuki) watakuwa wanaleta wataalamu wao hapa kwenye taasisi yetu, pia tumeomba mafunzo ambapo wataalamu wetu watapata fursa za kwenda kwao kujifunza ujuzi zaidi,” alisema.

Akizungumza, Profesa Ener alisema ziara yao hiyo ililenga kujionea uwekezaji uliofanywa ndani ya taasisi hiyo.

“Tumejionea hali halisi na tumeridhika kwamba Serikali imefanya kazi kubwa, tupo tayari kuleta timu za madaktari bingwa kuja kushirikiana nanyi, tutaenda kujipanga kwa suala hilo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles