26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Uturuki kujenga kituo cha Albino nchini

albinos-tanzania-schoolPatricia Kimelemeta na Asifiwe George, Dar es Salaam
TANZANIA kwa kushirikiana na Uturuki inatarajia kujenga kituo kikubwa cha albino ambacho kitakuwa na huduma mbalimbali muhimu ikiwamo shule na afya.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema kituo hicho kitawasaidia albino kupata huduma muhimu wakiwa kwenye mikono salama.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kumalizika kikao cha ndani cha mabalozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali.
“Rais Jakaya Kikwete alizungumza na Serikali ya Uturuki kuangalia jinsi tunavyoweza kuwasaidia wenzetu wenye ulemavu wa ngozi.
“Miongoni mwa makubaliano hayo ni kujenga kituo kikubwa cha walemavu hao ambacho kitakuwa na huduma mbalimbali ambazo ni pamoja na shule, kituo cha afya ambacho kitakuwa kinatoa huduma za matibabu kwa walemavu hao,”alisema.
Membe alisema kituo hicho kitakuwa na watalaam wa kutoa mafunzo mbalimbali pamoja na ulinzi ikiwa ni mkakati wa serikali kuhakikisha tatizo la mauaji ya albino linakwisha nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles