Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana leo na waziri wa mambo ya nje wa Iran aliyekwenda mjini Ankara kwa ajili ya kumpa taarifa rais huyo juu ya mkutano wake na rais wa Syria Bashar al Assad.
Uturuki inawaunga mkono waasi wa Syria na Iran inamuunga mkono rais Assad katika vita vya muda mrefu nchini Syria lakini pande zote mbili zimekuwa zikiwasiliana kufuatia juhudi za kimataifa za kutaka kuvimaliza vita hivyo.
Mazungumzo ya duru mpya kuhusu Syria yamepangiwa pia kufanyika nchini Kazakhstan Aprili 25-26 katika mji mkuu wa nchi hiyo Astana uliobadilishwa jina hivi karibuni na kuitwa Nur-Sultan. Mohammad Javad Zarif amewaambia waandishi habari kwamba alifanya majadiliano marefu na Rais Bashar al Assad na leo hii atatowa maelezo ya mjadala huo kwa rais wa Uturuki Tayyip Erdogan.