22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Warushiana vijembe bungeni

Mwandishi Wetu, Dodoma

Mbunge wa Jang’ombe, Ali Hassan King na Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji wamerushiana vijembe bungeni na kusababisha wabunge kuangua vicheko.

Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji, akirusha kijembe kwa Mbunge wa Jang’ombe, Ali Hassan King .
|Picha na Silvan Kiwale

Vijembe hivyo vilizuka mapema leo Alhamisi Aprili 18, wakati wabunge wakichangia Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bungeni Dodoma leo ambapo wakati Khatib akichangia alisema yeye ameenda kufanya kazi bungeni na kama King ameenda kuimba na kucheza taarabu ni yeye.

Baada ya kusema hivyo, ndipo King naye akapata nafasi ya kuchangia na kusema  mchicha una mwiba lakini unaliwa kama Khatib akitaka kuimba taarabu atumie kipaza sauti anachotumia yeye sio zake nyingine anazotumia mtaani.


Mbunge wa Jang’ombe, Ali Hassan King akijibu kijembe cha
Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji.

|Picha na Silvan Kiwale

Hata hivyo, haikueleweka wabunge hao walikuwa wanamaanisha nini lakini imekuwa ni kawaida kwao kurushiana vijembe pindi mmojwapo anapopata nafasi ya kuchangia ama kuuliza swali bungeni.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akicheka bungeni kutokana vijembe walivyokuwa wakirushiana wabunge.

|Picha na Silvan Kiwale
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles