25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

UTT AMIS: Watanzania wekezeni kwa manufaa ya baadae

*Yasema elimu zaidi bado inahitajika

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Ukosefu wa elimu ya mifumo ya imatajwa kuwa miongoni mwa changamoto kubwa inayowakabili watu wanaowekeza kwenye mifuko ya uwekezaji nchini.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 31, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa UTT Amis, Simon Migangala wakati wa mkutano na Wahariri na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya kampuni hiyo.

Amesema pamoja na kwamba kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa Watanzania kujitokeza kuwekeza na mifuko iliyo chini ya kampuni hiyo, lakini bado elimu zaidi inahitajika.

“Tunashukuru kwamba mifuko yetu yote imekuwa ikienda vizuri, lakini UTT Amis tunakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo watu wengi kukosa uelewa na elimu ya masoko ya fedha.

“Pia wengi bado hawana kipato kikubwa cha kuwekeza, mtu anaona kwamba kutumia fedha badala ya kuiwekeza kwa ajili ya malengo ya baadaye, tumezingatia shida zetu kuliko kuwekeza,” amesema Migangala.

Amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo watahakikisha kwamba wanatoa elimu zaidi kwa wananchi ikiwamo kutumia vyombo vya habari ili kujenga uelewa kuhusu mifumo hiyo ya uwekezaji.

Katika hatua nyingine amesema UTT Amis imeboreshwa kwa uwekezaji wenye malengo ya muda mrefu na muda mfupi ili kuhakikisha kila Mtazania anawekeza kwa maslahi yake na taifa kwa ujumla.

“Maisha yetu tunategemea fedha ikiwa tofauti na miaka ya zamani kwa wengi tulikuwa tunarithishwa aridhi lakini sasa hivi urithi wetu unategemea kwenye uwekezaji wa fedha hivyo niwahimize kuwekeza UTT AIMS kwani kila Mtanzania atajivunia,” amesema Mgangala.

Akizungumzia mafanikio ya miaka minne mfululizo waliopata kutokana na uwekezaji mdogo na mkubwa wameweza kuchangia katika Pato la Taifa.

“Mafanikio haya ni kwa mwaka juzi ukuaji wa taasisi kutoka Sh bilioni 600 hadi Sh bilioni 996 sawa na asilimia 50 kwa mwaka 2022 kutoka Sh bilioni 996 hadi Sh Trilioni 1. 5 sawa na asilimia 54 ukuaji huu umeenda vizuri ikilinganishwa na kipindi cha nyuma,” amesema Mgangala.

Amesema kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni, mwaka huu ukuaji umeongezeka kwa asilimia 12 kwa miaka sita huku wakitoa gawio kwa serikalini.

Aidha, amewataka Watanzania kuendelea kuwekeza kwasababu taasisi hiyo iko imara na kwamba kufanya hivyo ni fursa kwa maisha ya baadaye.

Naye, Mkurugenzi wa Masoko UTT Amis, Daud Mbaga amesema lengo lolote lazima liwe na muda katika kuwekeza kwenye fedha na mtaji.

Amesema kwa kiasi kikubwa wameweza kufanikiwa kutoa elimu vyuoni hadi shule ya msingi hivyo wawekezaji wengi ni wanafunzi, walimu na wengine.

“Watu waliofikiwa na elimu ya UTT Amis hatupimi kwa asilimia hivyo Tanzania inazaidi ya vijiji 3,000, hivyo tunakutana na watu mbalimbali kuhakikisha kwamba inamfikia kila mtu,” amesema Mbaga.

Amesema wanamkakati wa kuongeza somo la uwekezaji liingie shule ya msingi na na ngazi nyingine za elimu ili wanafunzi wajue umuhimu wa kuwekeza na faida na shughuli za UTT Amis.

Akifafanua zaidi amesema UTT Amis wamefanikiwa kujitanua zaidi katika kuhakikisha kuwa wanafika kwenye maeneo mengi wanakopatikana wawekezaji hususan Mikoa mbalimbali ya Tanzania.

“Tuna ofisi Arusha, Dodoma na Dar es Salaam na kiwngine pia tuna mawakala  nchi nzima kupitia matawi ya benki ya CRDB ambapo wawekezaji wetu wanapata huduma.

“Hapo awali ilimbidi mwekezaji wetu aende benki moja kwa moja ili kununua vipande, lakini kwasasa Mwekezaji anaweza kununua vipande kupitia njia zote za malipo za benki ya CRDB yaani Simbanking, CRDB App na Fahari Huduma.

“Pia kwa kutumia simu ya mkononi huduma za  Tigopesa, Airtel Money, M-Pesa, T-pesa na Halopesa inawezekana kununua vipande. Hali kadhalika kwa kutumia program tumizi (App) za benki ya Amana na  Standard Charter mwekezaji anaweza kununua vipande moja kwa moja. Hivyo ni bayana kuwa teknolojia imekuwa nyenzo muhimu katika kusaidia kuwafikia na kuwahudumia wawekezaji wetu kwa urahisi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles