23.5 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Uteuzi wa Ikulu pasua kichwa

Rais John Maguful
Rais John Maguful

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

UTEUZI wa Rais John Magufuli  wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya pamoja na makatibu tawala wa wilaya, sasa ni pasua kichwa.

Hali hiyo inatokana na baadhi ya majina ya wateule wa nafasi hizo kuonekana mara mbili katika nafasi tofauti jambo ambalo limezua mijadala katika mitandao ya  jamii kuhusu umakini wa maofisa wa Ikulu katika utekelezaji wa hatua hiyo

Miongoni mwa makosa yaliyofanywa na Ikulu jana ni uteuzi wa Dk. Leonard Massale ambaye alitangazwa jana kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma wakati tayari ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Kutokana na mkanganyiko huo, baadaye Ikulu ilitoa taarifa mbili tofauti ndani ya saa moja ikifafanua suala hilo la uteuzi.

“Tunapenda kufanya marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye orodha ya wakurugenzi wa halmashauri, majiji na manispaa ambako Dk. Massale ametangazwa kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma.

“Jina hilo limeingizwa katika orodha hiyo kwa makosa na kwa sababu hiyo, Dk. Massale anaendelea kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza na nafasi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma itatangazwa baadaye,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya Ikulu.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ilifafanua kuwa makatibu tawala wa wilaya, wote ambao majina yao yamejitokeza katika orodha ya wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali, Rais Magufuli ameamua kuwabadilishia majukumu na sasa watatumikia vyeo vyao vya ukurugenzi badala ya vyeo vya ukatibu tawala wa wilaya.

Kwa mujibu wa hiyo, nafasi za makatibu tawala wa wilaya ambao wameteuliwa kuwa wakurugenzi wa halmashauri nafasi zao zitajazwa baadaye.

Kubadilishwa ghafla kwa nafsi za uteuzi wa Rais, pia kulimkumba  Emile Ntakamulenga ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Uteuzi wake ulitenguliwa muda mfupi kabla ya kula kiapo cha maadili kwa wakuu wa wilaya Ikulu Dar es Salaam, Juni 30 mwaka huu, ikielezwa kuwa uteuzi huo ulikosewa na kwamba nafasi hiyo  ni ya Nurdin Babu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles