23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Nzoka: Narudi kuvaa kombati

Samuel Nzoka
Samuel Nzoka

NA MOHAMED HAMAD, KITETO

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Kanali Samuel Nzoka, amesema kamwe hajutii kutemwa katika nafasi hiyo na Rais Dk. John Magufuli.

Kanali Nzoka ambaye ni ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), alisema hiyo ni mipango ya Mungu, na sasa anajiandaa kurudi alikotolewa kabla ya kushika wadhifa huo.

Akizungumza na MTANZANIA mjini Kibaya hivi karibuni, Kanali Nzoka, alisema kabla hajateuliwa kushika wadhifa huo, alikuwa jeshini na kwamba anarudi kwa mwajiri wake wa mwanzo.

“Ingawa nina siku chache za kustaafu, narudi  kuvaa kombati, baadaye naomba likizo ya kustaafu nikapumzike, nimeitumikia nchi hii muda mrefu,” alisema.

Alisema kinachomkera ni upotoshwaji unaofanywa na vyombo vya habari, kuwa Rais Magufuli ameamua kuondoa wazee, watu wasioendana na kasi yake na wengine wakisema kufuta wateule wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

“Kuwa madarakani kunatokana na utashi wa bosi wako… siamini hata kidogo eti tumeondolewa kwa sababu tuliteuliwa na Kikwete… huo ni upotoshwaji mkubwa ambao unaweza kuligawa taifa letu.

“Tuamini huu ni uamuzi na utashi wa mteule, halazimishwi kuwa na watu ambao haoni umuhimu wake na katika utawala ni jambo la kawaida,” alisema Kanali Nzoka.

Kuhusu amani katika Wilaya ya Kiteto, Kanali Nzoka, alisema alipelekwa hapo kwa kazi maalumu ya kuhakikisha amani na uhusiano vilivyokuwa vimepotea kati ya wakulima na wafugaji vinarudi.

“Wilaya  hii ilipewa majina mengi mno, yakiwamo ya Kosovo, Darfur, Somalia kutokana na mauaji ya wakulima na wafugaji ambao kila kukicha kazi yao walikuwa wanagombea ardhi, napenda kusema sasa  hali ni shwari, najivunia hili.

“Zipo chokochoko za hapa na pale ambazo hazijaisha kabisa, anayechukua jukumu hili sasa namtaka awe makini,” alisema Kanali Nzoka.

Alisema migogoro ya Kiteto ina sura nyingi kwani tangu alipokabidhiwa wilaya hiyo, alihakikisha viongozi wa vijiji hawapati nafasi ya kuuza ardhi ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha migogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles