25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Utata Wimbo wa Taifa kuwekewa vikwazo taasisi za elimu

WANDISHI WETU

UTATA umeibuka kuhusu matumizi ya Wimbo wa Taifa katika taasisi za elimu nchini, kufuatia barua inayodaiwa kutolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupiga marufuku matumizi ya wimbo huo.

Barua hiyo inayoelekezwa kwa wakuu wa vyuo vya ualimu, wakuu wa vyuo vya maendeleo ya jamii, wakuu wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki na taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, inahimiza pia matumizi sahihi ya Bendera na nembo za Taifa.

Barua hiyo iliyoandikwa Novemba 23 mwaka huu ikiwa na kumbukumbu namba CHA-56/193/02/16, inasema wizara hiyo imepokea barua ya maelekezo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu matumizi sahihi ya bendera na Nembo ya Taifa, na Wimbo wa Taifa.

“Maelekezo haya yameletwa kwa sababu imebainika kuwa Taasisi za Serikali zinatumia isivyo sahihi alama za Taifa zilizotajwa hapo juu. Kwa makosa haya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inaelekeza kuwa Wimbo wa Taifa utapigwa kwenye dhifa za kitaifa pekee.

“Endapo hadhi ya sherehe haitambuliki, taasisi italazimika kuomba kibali kwa waziri mwenye dhamana. Wimbo unatakiwa kuimbwa kwa ukamilifu beti zote mbili kwa kuzingatia ‘nota’ na maneno (ona kiambatisho 1),” ilieleza sehemu ya barua hiyo.

Kuhusu rangi za Bendera ya Taifa, barua hiyo inaelekeza kuwa ni kijani, dhahabu, nyeusi na bluu na kwamba ni makosa kutumia rangi ya njano. Pia inaeleza kuwa uwiano wa bendera ni 2/3 kwa urefu a upana.

Akizungumzia barua hiyo jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo alieleza kushangazwa na kusambaa kwa barua hiyo aliyodai kuwa ni ya kiofisi.

“Ukiangalia watu walioandikiwa hiyo barua utajua kuwa siyo yenu. Hayo ni mawasiliano ya kiofisi,” alisema.

Hata hivyo hakutaka iuendeela kutoa ufafanuzi kuhusu barua hiyo inayoonekaa kupiga marufuku kuimbwa kwa Wimbo wa Taifa katika mikusanyiko isiyo rasmi, ikiwemo ya wanafunzi wanapokuwa kwenye gwaride la asubuhi ambako ndiko hupata nafasi ya kujifunza na kukariri wimbo huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles