KOMBA KAKOA NA LEONARD MANG’OHA |
MWENYEKITI wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo anadaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Nondo, ambaye pia Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), anadaiwa kutoweka jana usiku, muda mfupi baada ya kuandika kwenye mtandao kwamba yupo hatarini.
Ofisa Habari wa TSNP, Hellen Sisya na mzazi wa Nondo jana walizungumza na waandishi wa habari kuelezea kutoweka kwake na waliliomba Jeshi la Polisi lihakikishe anapatikana akiwa salama.
Sisya aliwaambia waandishi wa habari kuwa walianza kuwa na mashaka kuhusu usakama wa mwenyekiti wao alipoanza kujitoa kwenye makundi mbalimbali ya mtandao wa kijamii ya whatsapp.
Alisema, Nondo alianza kujitoa kwenye makundi hayo Machi 7, mwaka huu kati ya saa 6:00 na 8:00 usiku jambo ambalo liliwashangaza na kuwapa shauku ya ….
Kwa habari zaidi soma nakala yako ya MTANZANIA.