24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Utambuzi, uandikishwaji vitambulisho vya Taifa kuanza upya desemba 2016

h3h9417
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba

Serikali imesema utambuzi na uandikishwaji  wa vitambulisho  vya Taifa utaanza upya Desemba mwaka huu ili kusaidia kupunguza utitili wa vitambuliso .

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba , zoezi  hilo litasaidia kutoa suluhisho la kudumu la mishahara hewa kwa watumishi wa umma.

“Kuna watu wanatumia majina tofauti lakini kwa kutumia njia ya kielekrotoniki, alama za vidole zinatofautisha  tunaamini  kutumia alama za vidole ataendelea kutumbulika,”alisema Waziri Nchemba.

Amesema lengo la kufanya hivyo  kwenye vitambulisho  hivyo  vitasaidia maeneo mengi kama bodi ya mkopo, mifuko ya jamii pia anaamini kutakuwa na uhusiano mzuri.

Ameongeza kuwa baada ya zoezi la watumishi wa umma  wanakwenda kuendelea kutoa namba  za utambuzi kwa wananchi na  ‘data base’ tayari ipo waliyopewa na Tume ya Taifa  ya Uchaguzi (NEC).

“Taasisi zitatumia utambuzi huu na zaidi ya taasisi 35 zimeanza kutumia taarifa zake kutoka NIDA na zingine zaidi ya 70  zimeonyesha nia ya kutumia  taarifa hizo,”alisema.

Kwa upande wa NIDA, usahili  wa awali  walihakiki watumishi wa umma  nchi mzima wapatao laki 565,000 na wengine bado kutokana na sababu mbalimbali.

Hadi sasa wamesajili wananchi milioni 3,900,000 na vitambulisho vya taifa milioni 2,700,000 ambavyo tayari vimezalishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles