24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

UTAFITI: UMASKINI CHANZO CHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA

Hadija Omary, Lindi



Umaskini uliokithiri umetajwa kuwa chanzo cha wazazi wengi kutengana na kusababisha watoto kulelewa na mzazi mmoja katika familia nyingi za vijiji vya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Hayo yameelezwa na Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Liwale, Mary Ding’ohi katika kikao cha kuwasilisha taarifa ya utafiti wa mwaka 2012 uliofanywa na taasisi ya Repoa  kuhusiana na hali  ya umaskini ya wilayani humo.

“Ndoa nyingi za jamii ya wakazi wa Liwale zinapovunjika waathirika wakubwa ni watoto ambao wanajikuta wakilelewa na mzazi moja jambo linalosababisha watoto hao kutanga tanga,” amesema.

Kwa upande wake Mtafiti wa taasisi hiyo, Cornel Johari amesema katika utafiti walioufanya mwaka 2012 ulionyesha hali ya umaskini kupitia kwa mtu mmoja mmoja ulikuwa katika jamii hiyo ni mkubwa.

“Utafiti huu ulitokana na sensa ya watu na makazi 2012 na ile ya mapato na matumizi ya kaya (HBS) ambapo mwaka 2015 Waziri wa Fedha kupitia kitengo cha kuondoa umasikini (PED) ambapo waliipa kazi Repoa kufanya utafiti huo wa kuhusu hali ya uchumi nchini ambapo kwa Mkoa wa Lindi tulifanya utafiti wetu Wilaya ya Liwale,” amesema Johari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles