29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ushirikina waiponza Dodoma Jiji FC

NA MWANDISHI WETU

TIMU ya Dodoma Jiji, imetozwa faini ya sh 1,000,000 kwa kosa la kujihusisha na vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina wakati wa mchezo wao na Mbeya Kwanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania leo Oktoba 28,2021, ambapo baadhi ya maofisa wa timu hiyo wakilizunguka lango la upande kusini la mwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya, huku wakimwaga vitu vyenye asili ya unga.

Kamati ya Uendeshaji wa ligi katika kikao chake cha Oktoba 26,2021 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya ligi hiyo na kufanya maamuzi.

Pia Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Renatus Mayunga, amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya sh 1,000,000 kwa kosa la kutoa lugha za matusi na vitisho kwa mwamuzi wa akiba wa mchezo, Credo Mbuya.

Mchezaji wa Mbeya Kwanza, Joseph Majagi ambaye alioneshwa kadi nyekundu, amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya sh 1,000,000 kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Dodoma Jiji, Augustino Nsata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles