22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

WaterAid yakabidhi mradi wa maji wa Milioni 422 Babati

Na Mwandishi Wetu, Babati

SHIRIKA  lisilo la kiserikali la WaterAid,limekabidhi mradi wa maji wenye thamani ya Sh milioni 422 kwa kijiji cha Sangara Juu wilayani Babati mkoa wa Manyara.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Oktoba 28,katika mradi uliotekelezwa na Shirika hilo umefadhiliwa na Coca-Cola Foundation, ambayo ni mpango wa misaada wa kampuni ya Coca–Cola na People Post Code Lottery(PPL).

Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika hilo hapa nchini, Anna Mzinga,amesema mradi huo wa awamu ya pili umegharimu Sh milioni 422, utanufaisha wananchi zaidi ya 2,500 na kuwa umelenga kusaidia wananchi wa kijiji hicho kupata huduma za maji safi na salama.

Amesema miradi hiyo imelenga kuimarisha upatikanaji endelevu wa maji safi na salama ambapo wameanzisha vikundi vya watumia maji kwa kufuata na kuzingatia sheria na miongozi ya serikali.

Akizungumza katika  makabidhiano hayo kijijini hapo,Mkurugenzi Msaidizi Idara ya rasilimali za maji katika Wizara ya Maji, Pamela Temu, amewapongeza wadau hao wa maendeleo kwa kusaidia kupatikana kwa huduma hiyo muhimu.

Amesema Wizara hiyo imefurahishwa na namna ya utekelezaji wa mradi huo ulivyoweza kuhusisha taaluma mbalimbali kuanzia ubunifu,usanifu na utekelezaji.

Mkurugenzi huyo aliwataka wananchi hao kutunza miundombinu ya maji ili miradi hiyo iwe endelevu na kutunza vyanzo vya maji ikiwemo kuepuka ukataji miti unaochangia ukame sehemu nyingi.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho,Neema Daudi,alishukuru kukamilika kwa mradi huo na kuwa awali walikuwa wakiteseka kufuata huduma ya maji umbali mrefu katika vijiji vya jirani na kuwa kwa sasa itawasaidia kutumia muda mchache kupata huduma hiyo muhimu.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Babati,Mhandisi Felix Mollel,aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanalinda miundombinu hiyo ya maji ili iweze kuwanufaisha ambapo pia alipongeza Shirika hilo kwa namna walivyotekeleza mradi huo kwa ufanisi na kushirikiana nao.

Rais wa Coca Cola Foundation,Saadia Madsbjerg,amesema katika jitihada za kuhakikisha wanafanya mabadiliko barani Afrika,wanaendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali za mashirika ya misaada kuhakikisha yanatekeleza miradi yenye manufaa kwa jamii.

“Mradi huu unaotekelezwa wilayani Babati ni mfano unaoonyesha jinsi ambavyo misaada ya kimkakati inaweza kuhakikisha watu wanapata maji katika maeneo ya pembezoni barani Afrika,”amesema Rais huyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles