29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Usambazaji umeme vijijini kuchochea maendeleo Katavi

Na CHELSEA TILLYA (UDSM)

TANGU Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, imekuwa ikisisitiza kuwa nchi hii ni lazima iwe ya viwanda.

Ili kufikia malengo hayo, Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akisema kwamba ni lazima nchi iwe na umeme wa uhakika, maeneo yote hata ya vijijini.

Kwa kutekeleza malengo hayo, imekuwa ikifungua miradi ya kuhakikisha inasambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya nchi ili viwanda viweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Mbali na sekta ya viwanda, serikali imekuwa ikifanya jitihada hizo ili kuhakikisha pia sekta nyingine za kijamii kama vile afya, elimu na nyinginezo zikiwa katika hali bora.

Kwa kupitia miradi hiyo, vijiji vya Mkoa wa Katavi, ni miongoni mwa vitakavyonufaika na miradi hiyo, baada ya Serikali kuingia makubaliano na Kampuni kutoka nchini China, China Railway Constraction Electrification Bureu Group Co.Ltd, (CRCEBG), ili kuhakikisha wananchi wa mkoa huo wanapata umeme ndani ya muda wa miaka miwili. Mwakilishi wa kampuni hiyo, Jonny Han, pamoja na mambo mengine, anasema kampuni yao imejipanga ili kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo wanapata umeme wa uhakika katika muda uliopangwa.

Anasema tangu waliposaini mkataba Machi mwaka huu, baada ya kupata malipo ya awali kutoka kwa wasimamizi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini, (REA), wameshasambaza umeme katika vijiji saba na mwezi huu watasambaza kwenye vijiji vingine kama vile Majimoto.

Anasema wao wanatambua jinsi wananchi wa maeneo hayo walivyo na hamu ya kupata umeme.

Anasema mbali pia wanafahamu jinsi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoyajali maisha ya wananchi wake.

“Tunatambua hamu ya wananchi kupata umeme, tunafahamu pia jinsi serikali inavyojali maisha ya wananchi wake. Kampuni itafanya bidii kuharakisha utekelezaji wa umeme wao,” anasema Han.

Anavitaja baadhi ya vijiji ambavyo vimeshanufaika na mradi huo kuwa ni Kapalala A&B, Kilida, Society, Ntibili, Mchakamchaka na Ifukutwa. 
” Tuna uhakika kuwa tunaweza kuwawezesha watu wengi kutumia umeme haraka iwezekanavyo,” anasema Han.

Anasema kwa sasa mradi huu unasimamiwa na REA na Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) ili kuhakikisha unakuwa kwenye ubora na viwango vinavyotakiwa.

Kuhusu suala la ajira kwa Watanzania, anasema wamewapa fursa wafanyakazi zaidi ya 90 wakiwa chini ya wahandisi wanne raia kutoka nchini kwao wakishilishirikiana na Watanzania kwa ajili ya manufaa ya taifa hili.
Anaipongeza Serikali ya Mkoa wa Katavi kwa jinsi walivyowapa msaada baada ya kupokea mradi huo.

“Tunaishukuru Serikali ya Mkoa wa Katavi kwa msaada ambao wamekuwa wakitupa tangu mradi huu uanze,” anasema mwakilishi huyo.
Anasema tangu waanze kazi hiyo, Serikali ya mkoa huo imekuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha kazi zao zinakwenda vizuri.

Anasisitiza kwamba kutokana na uzoefu walionao kupitia kwenye miradi mbalimbali ambayo wamewahi kuifanya katika mataifa mbalimbali duniani, watahakikisha hawawaangushi.

Anasema ana matumaini baada ya mradi huo kukamilika maisha ya wakazi wa maeneo hayo yatakuwa bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles