Usafirishaji wa mfereji wa Suez kurudi kwenye hali yake ndani ya siku 4

0
446

Cairo, Misri

Mkurugenzi wa Mamlaka ya mfereji wa Suez (SCA), Osama Rabie amesema, usafirishaji kupitia mfereji wa Suez unatarajia kurudi kwenye hali ya kawaida ndani ya siku 4.

Rabie amesema kutokana na kuinuliwa na meli iliyokuwa imekwama, mfereji wa Suez ulianza tena usafirishaji jana, ambapo meli 113 zimepita. Amesema kazi ifuatayo ya SCA ni kutatua suala la msongamano.

Rabie pia amesema ukaguzi wa hatua ya mwanzo kwenye tukio hilo umeonesha kuwa halina tatizo lolote la kiufundi kwenye meli hiyo. Meli hiyo itakaa katika eneo la bahari ya Misri mpaka matokeo ya mwisho ya uchunguzi kutolewa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here