31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Sarah Obama azikwa Kogello, nchini Kenya

Nairobi, Kenya

Sarah Ogwel Onyango Obama, Bibi yake, aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani Barack Hussein Obama amepumzishwa nyumbani kwake kijijini Kogello jimboni Siaya, Nyanza, Magharibi mwa Kenya.

Katika mazishi hayo ambayo hayakuhudhuriwa na wakaazi wengi wa sehemu hiyo kutokana na kanuni za serikali kupiga marufuku mikusanyiko mikubwa ya watu, yameendeshwa kwa mujibu wa itikadi za dini ya Kiislamu.

Kwenye mazishi hayo, ujumbe wa salamu za rambirambi za waombolezaji, ukiwemo wa Rais Uhuru Kenyatta uliosomwa na Waziri wa nchi za kigeni Rachael Omamo.

Mama Sarah ameendelea kukumbukwa kama mfanisi mkubwa wa miradi ya maendeleo katika jamii pamoja na kujitolea kwake kuwasaidia wasiojiweza akichangia kwa kiasi kikubwa  katika sekta ya elimu. 

Mama Sarah Obama alikuwa mke wa Babu yake Barack Obama, Jaduong Hussein Onyango Obama ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1870 na kufariki tarehe 29 Novemba mwaka 1975. 

Mama Sarah Obama, alitambulika zaidi duniani baada ya mjukuu wake Barack Obama alichaguliwa kuwa seneta wa jimbo la Illinoise – Marekani, kabla ya kushinda uchaguzi na kuwa Rais wa 44 na Rais wa kwanza mweusi wa taifa hilo kubwa duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles