Urusi yakanusha kuhusika na udukuzi wa wizara Marekani

0
387
MOSCOW, RUSSIA - NOVEMBER 23, 2019: Russia's President Vladimir Putin addresses the 19th conference of the United Russia Party at the VDNKh Exhibition Centre. Alexei Druzhinin/Russian Presidential Press and Information Office/TASS (Photo by Alexei DruzhininTASS via Getty Images)

MOSCOW, URUSI

Ikulu ya Kremlin imesema leo Desemba 15, kuwa Urusi haikuhusika kabisa na udukuzi uliofanyika katika wizara za fedha na biashara nchini Marekani.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amepuuzilia mbali madai yote yaliyoihusisha Urusi na tukio hilo akisema Rais Vladimir Putin ndiye aliyeipendekezea Marekani kukubali na kumaliza makubaliano ya usalama wa kimtandao na Urusi.

Watu walio na taarifa za ndani kuhusiana na udukuzi huo wameliambia Shirika la habari la Reuters kuwa wadukuzi wanaaminika kuifanyia kazi serikali ya Urusi na kuna hofu kwamba udukuzi huo uliofanyika sasa ndio mwanzo tu wa mkoko kualika maua.

Mtu mmoja anayehusika na suala hilo anasema udukuzi huo ulikuwa mkubwa kiasi cha kwamba ulisababisha kufanyika kwa mkutano wa Baraza la Kitaifa la Usalama katika ikulu ya Marekani White House Jumamosi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here