28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Rais wa Iran asema Israel ndiyo iliyomuua mwanasayansi wake

TEHRAN, IRAN

Rais wa Iran, Hassan Rouhani amesema kuwa Israel ndiyo iliyohusika na mauaji ya mwanasayansi aliyeanzisha mpango wa nyuklia wa jamhuri hiyo ya kiislamu katika miaka ya 2000.

Rouhani anasema Israel ilimuua ili ianzishe vita katika siku za mwisho za utawala wa Rais Donald Trump.

Matamshi haya ya rais huyo wa Iran ndiyo ya kwanza yanayoLituhumu taifa hilo la Kiyahudi moja kwa moja na mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh mwishoni mwa mwezi uliopita.

Israel ambayo kwa muda imeshukiwa kuhusika na mauaji hayo imekanusha kulizungumzia suala hilo. Rouhani ameapa kulipiza kisasi ila amesema hatokubali Israel iichagulie wakati na pale itakapofanya shambulizi hilo. Amesema Iran haitokubali kuyumba kwa usalama katika kanda ya Mashariki ya Kati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles