32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Urusi yajitosa kufufua uchumi wa Libya

MOSCOW,Urusi



SERIKALI ya nchi hii imesema   ipo tayari kuimarisha uchumi wa Libya pamoja na huduma za jamii nchini humo.

Hayo yamesemwa jana na Waziri Mkuu wa nchi hii,  Dmitry Medvedev katika mkutano wa siku mbili uliofanyika nchini Italia kwa ajili ya kujadili hatma ya Libya.

Alisema kwa sasa nchi hiyo inahitaji msaada wa haraka kuimarisha uchumi wake na nyanja zoe za jamii jambo ambalo litakuwa ufunguo mpya wa maisha ya wananchi nchini humo.

“Panahitajika kuimarisha hali ya uchumi, kurejeshwa  nyanja ya jamii, miradi  ambayo nchi hiyo inaahidiwa inapaswa kutolewa  – hii pia itakuwa ni ufunguo wa upya wa maisha ya kawaida nchini Libya,” alisema waziri mkuu  huyo.

“Na sisi tupo tayari kushiriki katika hilo,” aliongeza.

 Medvedev alisema nchi hii ina uzoefu mkubwa  wa ushirikiano  kimataifa katika masuala  kama hayo ikiwa ni pamoja wanavyoshirikiana katika kutatua mgogoro wa  Syria.

“Aina hii inaonyesha yenye ufanisi hata katika hali ngumu,” alisisitiza.

 Alisema pamoja na hali ngumu lakini wanakaribia kuutatua mgogoro.

“Mikataba ya siasa ni kama ncha ya barafu,” alisema waziri mkuu huyo.

“Kwa sababu baada ya kufikiwa makubaliano hayo ya siasa  linalofuata ni uchumi ulioharibiwa  na makundi mbalimbali ambayo yanajaribu kuua  uwezo wa nchi ambayo ilikuwa ni moja ya mataifa tajiri,  basi mikataba yote ya siasa inatakiwa kutekelezwa kwa haraka au baadaye,” aliongeza waziri mkuu huyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles