28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

URUSI; TUNAFUATILIA KWA KARIBU OPERESHENI ZA UTURUKI

MOSCOW, UrusiSERIKALI ya Urusi imesema inafuatilia kwa karibu operesheni zinazoendeshwa na Uturuki katika eneo la Afrin lililopo Kaskazini Magharibi mwa Syria.

Taarifa hiyo imetolewa jana mjini hapa na Msemaji wa Rais, Dmitry Peskov katika mkutano wake na waandishi wa habari.

“Bado tunafuatilia kwa karibu maendeleo ya operesheni katika eneo la Afrin, Syria. Wawakilishi wa Urusi wanaendelea kuwasiliana na uongozi wa Syria na Uturuki juu ya suala hilo,” alisema msemaji huyo.

“Hakika tunafuatilia suala hili kwa karibu hasa kuhusu masuala ya haki za bindamu kuhusu matukio ya sasa katika eneo hilo la Afrin hususani operesheni za Uturuki,” aliongeza msemaji huyo.

Hata hivyo, Peskov alikwepa kujibu swali kama Serikali ya Moscow inafahamu Uturuki inajiandaa kuendesha oparesheni kubwa zaidi eneo hilo.

Taarifa hiyo ya Urusi imekuja baada ya Januari 20 mwaka huu Jeshi la Uturuki kutangaza mpango wa kuendesha opresheni waliyoipa jina la ‘Olive Branch’ dhidi ya wapiganaji wa Kikurd na wafuasi wa Chama cha Democratic Union waliopo eneo hilo lenye wakazi milioni 1.5.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, ndege za Uturuki zimesharusha makombora yapatayo 153 katika eneo hilo.
Taarifa za kituo cha televisheni cha Sky News Arabia zinaeleza kuwa ndege hizo zilisababisha vifo vya raia sita na wapiganaji watatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles