25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Urusi, Philippines zatangaza kuondoka ICC

rogrigo-duterteMANILA, PHILIPPINES

RAIS wa Philippines, Rogrigo Duterte, jana amesema huenda akafuata nyayo za Urusi iliyotangaza juzi kuondoa saini katika mkataba unaounda Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Alitangaza hatua hiyo wakati akigusia ukosoaji unaofanywa na mataifa ya magharibi juu ya vita yake ya mauaji ya wahalifu wa mihadarati.

Duterte ameielezea ICC kama mahakama ‘isiyo na maana’ na kuonyesha kufedheheshwa na madai ya mataifa ya Magharibi kuwa anafanya mauaji kinyume cha sheria, akisema wanashindwa kuelewa sababu za kuwaua watuhumiwa.

Rais huyo pia ameulaumu Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kukabiliana na vita duniani kote.

Hatua yake hiyo imekuja baada ya Urusi kutangaza kuondoa saini yake katika mkataba ulioanzisha ICC kwa kile ilichodai kuendeshwa kwa upande mmoja.

“Mahakama imeshindwa kufikia matarajio yake na imeshindwa kuonyesha hali ya kujisimamia yenyewe badala yake yake inaburuzwa,” Wizara ya Mambo ya Nje ilisema katika taarifa yake.

Pamoja na kwamba Urusi ambayo imechukua hatua hiyo kwa amri ya Rais Vladimir Putin si mwanachama wa ICC, ilitia saini mkataba uliosababisha kuundwa kwa mahakama hiyo.

Urusi na Philippines ni mataifa ya mwanzo nje ya Afrika kuchukua hatua hiyo baada ya Gambia, Afrika Kusini na Burundi kufanya hivyo.

Viongozi wa Afrika wamekuwa wakilalamika kuandamwa zaidi na ICC, huku mataifa makubwa yakiwa hayaguswi.

Philippines ilijiunga na ICC mwaka 2011 na mwezi uliopita mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama hiyo, alisema mahakama inaweza kuwashtaki wanaofanya mauaji katika nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles