28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Uropokaji wamponza Jerry Muro

muroNA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) iliyokutana Mei 5, mwaka huu, imempiga faini ya Sh 5,000,000, Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Jerry Muro, kwa kutoa kauli za chuki, kisirani na uchochezi dhidi ya uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB) nchini na TFF.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, Muro alitoa utetezi wake mbele ya Kamati ya Nidhamu kukiri na kujutia kufanya kosa hilo na kudai ilitokana na ugeni wake katika uongozi wa michezo, kwa kuzingatia hilo kamati ilimuepusha na adhabu ya kufungiwa.

Kwa mujibu wa Ibara ya 53 (2) ya Kanuni za Nidhamu za TFF toleo la 2012, kwa kuidhalilisha TFF na Bodi yake ya Ligi mbele ya umma, kamati imemtoza faini ya Sh 5,000,000 Jerry Muro na kuwaonya viongozi wengine wa familia ya mpira wa miguu kutojihusisha na vitendo vya matamshi ya aina hiyo.

Shitaka linalomhusisha mchezaji wa Yanga, Amissi Tambwe kumshika kwa kumdhalilisha mchezaji wa Simba SC, Juuko Mursheed na kiongozi wa Friend Rangers, Hery Chibakasa kuhamasisha vurugu katika mchezo wa timu yake na dhidi ya Majimaji ya Songea, Januari 29, 2015, kamati imeahirisha mashitaka hayo mpaka tarehe nyingine itakapopangwa.

Kamati iliahirisha malalamiko dhidi ya Mohamed Hussein, Muhibu Kanu, Manfred Luambano, Venance Joseph, Mussa Senyange, Saleh Ali, Shafii Maganga na Ismail Salim baada ya kupokea taarifa za udhuru zilizosababishwa na mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria ya mikoani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles