27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanasheria TTF kutinga Toto Africa

NA JUDITH NYANGE, MWANZA

MWANASHERIA wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Emmanuel Muga, anatarajia kuhudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa klabu ya Toto African ya mjini hapa, utakaofanyika Mei 23 mwaka huu, baada ya mkutano wa awali kuvunjwa na wanachama.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassan Kilaka, alisema katika mkutano wa awali uliofanyika Mei 3, mwaka huu, ulivunjika kutokana na migogoro iliyoibuka baina ya wanachama na uongozi wa klabu hiyo.

“Katika mkutano wa awali baadhi ya wanachama walitaka kupindua uongozi wa klabu ya Toto, wengine walikuwa na katiba ambayo haitambuliki na klabu na kusababisha mkutano huo kuvunjika,” alisema Kilaka.

Kilaka alisema wameamua kuwaalika TFF kuja kutatua mgogoro huo uliopo ndani ya klabu hiyo baina ya wanachama na uongozi wa klabu, kabla ya kuanza kwa Ligu Kuu, ili kuiepusha timu hiyo kukumbana na matatizo kama yaliyotokea mwaka 2007.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2007 baada ya klabu hiyo kupanda daraja, kundi dogo la wanachama walifanya mapinduzi na kupindua uongozi wa klabu hiyo na kupelekea klabu hiyo kushindwa kufanya vizuri na kushuka daraja.

Kilaka amewataka wanachama wa klabu hiyo wajifunze kulingana na yaliyotokea mwaka 2007, waachane na vurugu wanazozianzisha kipindi timu hiyo inapopanda daraja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles