24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Urais 2025 waliponza Gazeti la Uhuru

Na MWANDISHI WETU

Serikali  imesitisha leseni  ya uchapishaji na usambazaji  wa  Gazeti la Uhuru kwa siku 14 kuanzia Agosti 12, 2021, likidaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo Jumatano, Agosti 11, na  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Gerson Msingwa, uamuzi wa  kusitisha leseni ya gazeti hilo, ni kutokana na  kuchapisha habari katika ukurasa wa mbele  wa toleo namba 24084 inayosema ‘Sina wazo kuwania urais 2025-Samia’.

Taarifa hiyo imesema ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari imebaini kuwa Habari hiyo ina upungufu upungufu wa kisheria na weledi wa taaluma kinyume na kifungu cha 50(1)(a),(b)na (d) na kifungu 52(d)na (e) vya sheria ya  huduma ya Habari Na.12 ya 2016.

“Rais Samia Suluhu Hassan hajatoa matamshi yoyote ambayo yanaeleza kutokuwa na wazo la kuwania urais mwaka 2025.

“Kwa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 9(b) cha Sheria ya Huduma za Habari Na 12 ya 2016, nimeamua kusitisha kwa muda wa siku 14 leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti la Uhuru kuanzia tarehe 12 Agosti, 2021.

“Pia kwa mujibu wa kifungu cha 10(1) cha Sheria ya Huduma za Habari Na 12 ya 2016 ikiwa gazeti la Uhuru halitaridhika na uamuzi wa Mkurugenzi  wa Idara ya Huduma za Habari linayo haki ya kukata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana ya Habari,” amesema Msigwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles