31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Uraia pacha wakataliwa

Bunge
Bunge

Na mwandishi Wetu

RASIMU ya Katiba inayopendekezwa imezika rasmi suala la uraia pacha. Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mjadala kuhusu uraia pacha, huku Watanzania wanaoishi nje wakishinikiza kiwepo kipengele kwenye Katiba kinachoruhusu suala hilo.

Akiwasilisha rasimu hiyo jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba, Andrew Chenge, alisema hakutakuwa na uraia pacha isipokuwa watu wenye asili ya Tanzania ambao hawana uraia watapewa hadhi maalumu.

“Kamati ya Uandishi ilifanya utafiti katika Katiba za nchi nyingine kama za India na Ethiopia na imebaini wao huwapa watu wenye asili ya nchi zao hadhi maalumu na kuwawezesha kupata haki mbalimbali,” alisema Chenge.

Hivyo alisema watu wenye asili ya Tanzania ambao waliacha kuwa raia wa Tanzania na kupata uraia wa nchi nyingine watatambuliwa na kupewa hadhi maalumu.

Kwa mujibu wa Chenge, haki hizo ni pamoja na kutohitaji viza za kuingia na kutoka na kukaa nchini miezi saba bila kuhitaji huduma za uhamiaji.

Hata hivyo, alisema hawataruhusiwa kupiga kura, kugombea nafasi yoyote ya kisiasa wala kushika madaraka ya utawala, kumiliki mashamba ya kilimo au kuwa na makazi.

“Kwa mantiki hiyo, fursa mbalimbali zinazofikiriwa kuwa zitapatikana kwa kuwapo kwa uraia pacha zinaweza pia kupatikana bila ya kuwapo kwa uraia pacha,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Hakuna mtu aliyeacha uraia wa Tanzania, ni katiba ya Tanzania ambayo inamzuia mtu kuwa raia wa Tanzania
    baada ya kupata uraia mwingine, sasa kama unatoa hati maalum kweli ili Bunge linaona
    kutolipa visa ndio cha msingi saana, unatoa hati maalum lakini unamzuia kukaa zaidi
    ya miezi saba, hawezi kumiliki shamba au makazi sasa atashiliki namna gani katika
    maendeleo ya nchi, kila siku tunapiga kelele tunataka wawekezaji wa mashamba na tunawapa
    ardhi lakini watanzania walio nje hawaruhusiwi.
    Nchi itaendelezwa na watanzania wenyewe kubaguana au kutunga sheria kwa misingi ya chuki
    badala ya kujenga Taifa hatutafika mbali, hili sio suala la sisi na wale, hili ni suala
    la watanzania wote na vizazi vijavyo tuwape nafasi waweze kushiriki na kutumia nafasi wanazopata
    kujiendeleza ili waendeleze Taifa, tusiwafunge vijana mikono na kutumia nafasi wanazopata kikamilifu.
    ndege akipaa lazima atatua, nyumbani ni nyumbani, chochote alichopata au atakochopata kitarudi
    nyumbani kwa njia moja au nyingine sasa kutoruhusu mtu amiliki chochote ni kichaa au ujinga ambao
    unabidi kushughulikiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles