24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Upinzani wasitisha kampeni za uchaguzi

LAGOS, NIGERIA

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Nigeria kimetangaza kusitisha kwa muda wa saa 72 kampeni yake ya uchaguzi wa urais kikipinga hatua ya Rais Muhammadu Buhari kumsimamisha kazi jaji mkuu wa nchi hiyo ambayo imetajwa kuzua mgogoro wa kikatiba.

Buhari, jana alisema amemsimamisha kazi Walter Onnoghen ambaye ametakiwa kufika mbele ya jopo la uchunguzi kufuatia madai ya kukiuka sheria za kuweka wazi mali kama tume maadili ya utumishi inavyoagiza.

Onnoghen hajayajibu madai hayo na mawakili wake wanasema jopo hilo halina mamlaka ya kumfungulia mashtaka.

Buhari aliyekuwa kiongozi wa kijeshi katika miaka ya 1980 na ambaye alichaguliwa kama rais mwaka 2015 anatafuta kuchaguliwa kwa mara nyengine katika uchaguzi utakaofanyika Februari 16.

Mpinzani mkuu wa Buhari katika uchaguzi huo, aliyekuwa makamu wa rais Atiku Abubakar, alimtuhumu rais kwa kitendo hicho alichokiita kuwa cha kidikteta na kisichokuwa halali.

Nacho Chama cha Wanasheria nchini Nigeria kimelaani vikali hatua hiyo kwa kusema kuwa ni jaribio la mapinduzi dhidi ya katiba.

Kuachishwa kazi kwa Walker Nkanu Samuel Onnoghen kumekuja wakati jaji huyo mkuu alikuwa akijiandaa kuwaapisha majaji wa mahakama za kesi za uchaguzi.

Onnoghen anakabiliwa na kesi ya madai ya kushindwa kutangaza mali za fedha za kigeni kama wanavyotakiwa kufanya maafisa chini ya sheria ya Nigeria.

Madai hayo yaliibuka wiki mbili zilizopita. Idara ya mahakama na jaji mkuu watatekeleza jukumu muhimu ikiwa kutatokea utata katika uchaguzi.

Buhari amesema hatua hiyo ya kusitishwa kazi itaendelea hadi pale kesi dhidi yake itakapokamilika. Hii ni mara ya kwanza kwa jaji mkuu kushtakiwa nchini Nigeria, ambako ufisadi umekithiri. Hata hivyo Onnoghen amesema kuwa mashitaka hayo hayana msingi.

Waangalizi tayari wameonya kuwa uchaguzi huo huenda uksababisha machafuko

Taarifa ya Buhari imesema kuwa mbali na mashitaka hayo ya Onnoghen, mashirika ya usalama yamegundua biashara nyingine inayotilishwa shaka ya mabilioni ya dola kwenye akaunti zake za benki.

Jaji Ibrahim Tanko Muhammed ameteuliwa kuchukua wadhifa wa kaimu jaji mkuu. Muhammed,  kama tu rais, anatokea upande wa kaskazini wenye Waislamu wengi, wakati Onnoghen anatokea kusini ambako kuna Wakristo wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles