Na Mwandishi Wetu,
WATAALAMU wa masuala ya lishe wanaeleza kwamba, watu wenye matatizo ya kupatwa na majipu, uvimbe na vidonda mara kwa mara huwa na upungufu wa virutubisho muhimu, ambavyo vinaweza kupatikana ndani ya papai.
Kwa kawaida papai husaidia kuleta nuru ya macho, pia husaidia kupunguza madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
Hivyo, wavutaji wa sigara ni vyema wakatumia tunda hili mara kwa mara ili kujipunguzia madhara ya moshi wa sigara.
Ni wazi kuwa papai ni tunda lililosheheni kila aina ya utajiri wa vitamin kuliko matunda mengine, ndani yake utapata vitamin A, B, C, D na E.
Wataalamu wa tiba za asilia wanaeleza kwamba tunda hili linaouwezo wa kutibu tatizo la usagaji wa chakula tumboni, pia hutibu kisukari na pumu na mara nyingine hata kifua kikuu.
Tunda la papai lina faida nyingi kwa afya ya mwanadamu.
Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda.
Pia yanasaidia kutibu kidonda cha moto.
Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani).
Pia husaidia kutofunga choo, maganda ya tunda la papai husaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.
Ukitafuna mbegu 10 – 12 kwa siku tano unaweza kutibu ini.
Majani yake ukiyakaushia ndani, yanaweza kutibu pumu. Inapoanza kubana, yachome kisha jifukize, kule kubanwa kutaisha.
Pia yanasaidia kutibu shinikizo la damu.
ukimeza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara tatu kwa siku kama ulikuwa na homa inakwisha.
Ukizikausha ndani, kisha zikasagwa na kuwa unga, zinasaidia kutibu malaria.
Tumia kijiko kimoja cha chai, changanya na uji, kunywa mara tatu kwa siku tano.
Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita mbili na nusu kwa dakika 15, yanatibu figo, Â na kuzuia kutapika. Kunywa nusu kikombe cha chai kutwa mara tatu kwa siku 5.