23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Una umri zaidi ya 50? Mwangalie Hillary Clinton

clinton

NA AGATHA CHARLES,

NI siku moja imebaki kwa wananchi wa Marekani kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo, baada ya utawala wa Rais Barack Obama kukoma.

Jarida la Rose haliko nyuma nalo linamtupia jicho mmoja wa wagombea urais nchini humo anayepigiwa mfano hasa kwa wanawake kuanzia aina ya mitindo ya mavazi na uongeaji.

Huyo si mwingine bali ni Hillary Clinton (69), ambaye baadhi ya mitandao ya masuala ya urembo huko Ulaya na kwingineko duniani inamwona kama nembo ya mitindo hasa kwa wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 50.

Licha ya mgombea huyo kuwa na umri Mkubwa, hata hivyo amekuwa kivutio katika mtindo wake wa uvaaji suti ambalo limekuwa vazi lake kuu na nembo yake katika mwonekano.

Suti zake za rangi tofauti amekuwa akizivaa sehemu mbalimbali, ikiwamo kwenye kampeni na hata katika dhifa za kidunia.

Wapo wanaomwita Hillary kama nyota  mwanamitindo wa siri kutokana na kupendeza kwa aina ya vazi lake ambalo hubuniwa kwa mwonekano tofauti tofauti.

Rangi anayoipenda zaidi Hillary inaelezwa kuwa ni njano inayomaanisha furaha na busara.

Wakati wote wa kampeni, watu wanaomuunga mkono walitengeneza akaunti ya Instagram inayojulikana kama hillarystreetstyle ambako watu waliiga mavazi yake na kutupia katika ukurasa huo kuonyesha kumuunga mkono.

Wanamuziki kama Beyonce Knowles, Kim Kardashian, Victoria Beckam, Angelina Jolie n.k wamekuwa wakitupia picha wakiwa wamevaa nguo zinazofanana na za mgombea huyo katika akaunti hiyo.

Wanawake wengi wanapofikia umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea hupata shida kujua staili yao ya mavazi itakayowafanya waonekane nadhifu, huku  wakienda na wakati kulingana na umri wao, sasa wanaweza kujaribu staili ya Hillary.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles