27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

UN yazindua mkakati mpya wa tabianchi

NEWYORK, MAREKANI 

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amezindua mpango mpya wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchini, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mazingira ulimwenguni.

Chini ya kauli mbiu ya ”mbio za kuelekea kiwango sifuri” juhudi hiyo mpya inanuwia kufanikisha lengo la kukomesha utoawaji gesi ukaa zinazochafua mazingira ifikapo mwaka 2050.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, karibu kampuni 1,000, miji 458, vyuo vikuu 500, majimbo na mikoa 24 pamoja na wawekezaji wakubwa 36 wameridhia kuunga mkono pendekezo la kufikia kiwango sifuri cha utoaji gesi chafuzi kwa mazingira ifikapo 2050.

Miongoni mwa kampuni zinazojiunga na kampeni hiyo ni pamoja na Rolls-Royce, Nestle na kampuni kubwa ya mitindo ya Inditex. 

Zaidi ya nchi 120 duniani pia zimeridhia mpango huo wa kuwa na ulimwengu bila gesi chafuzi ifikapo katikati ya karne ya 21.

Rais wa mkutano ujao wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi ambaye pia ni waziri wa nishati wa Uingereza, Alok Sharma, amesema hapo kabla kuwa shughuli za uchumi ulimwenguni zinapaswa kufanyiwa mageuzi ya kuwa endelevu na zisizochafua mazingira baada ya kumalizika kadhia ya janga la corona.

Shama amesema kampeni mpya ya Umoja wa Mataifa ya kufikia kiwango sifuri ni sharti izihimize kampuni na serikali duniani kuonesha nia ya kulinda mazingira na hali ya hewa.

Waziri wa nishati wa Uingereza Alok Sharma amesema kuna haja ya kufanyika mageuzi makubwa katika sekta za kiuchumi.

Majanga ya asili yatokanayo na hali ya hewa yameonesha kile ambacho kinaweza kutokea duniani ikiwa kiwango cha joto katika uso wa sayari ya dunia hakitadhibitiwa.

Vimbunga kama vilivyotokea eneo la Afrika Mashariki, moto wa nyika uliozitia kishindo Australia na Marekani pamoja na kupungua kiwango cha barafu kwenye ncha mbili za ulimwengu ni kati ya madhara yatakayojitokeza.

Kulingana na jukwaa la mabadiliko ya tabia nchi la Umoja wa Mataifa, kiwango cha joto katika uso wa dunia kimepanda kwa nyuzi moja ikilinganishwa na kabla ya enzi ya mapinduzi ya viwanda na kwamba miaka minne iliyopita imekuwa na hali ya joto kuliko ilivyowahi kushuhudiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles