23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Chupa za plastiki, mirija marufuku Kenya

NAIROBI, KENYA

KENYA Kenya imepiga marufuku matumizi ya plastiki kama vile chupa za maji na mirija katika mbuga zake za wanyama, fukwe na misitu na maeneo mengine yanayohifadhiwa.

Utekelezaji wa marufuku hiyo iliyotangazwa mwaka mmoja uliyopita, umeagizwa kupitia barua kutoka kwa Waziri wa Utalii, Najib Balala wiki iliyopita, na ulianza jana, miaka minne tangu Kenya ilipotangaza moja ya marufuku kali zaidi duniani kuhusu matumizi ya mifuko ya plastiki.

Shirika la programu ya mazingira za Umoja wa Mataifa UNEP, linakadiria kwamba zaidi ya tani milioni 8.3 za plastiki zimezalishwa kila mwaka duniani tangu mwanzoni mwa miaka ya 1950, ambapo karibuni asilimia 60 inaishia kwenye madampo au mazingira ya asili.

UNEP imesema katika taarifa kwamba kwa kupiga marufuku plasitiki za matumizi ya mara moja kwenye mbuga za taifa na maeneo yanayohifadhiwa, Kenya imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kushughulikia janga na dunia la uchafuzi wa plastiki.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles