Bamako, Mali
Umoja wa Mataifa nchini Mali (UN) umetuma ujumbe wa kuachiwa huru mara moja kwa Rais wa Mali, Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane baada ya kutolewa taarifa ya kuzuiliwa na wanajeshi.
Katika ujumbe huo ulioandikwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwa lugha ya kifaransa pia umetoa wito wa utulivu katika taifa hilo la Afrika magharibi.
Kauli hiyo imetokana na ripoti ya kwamba Rais wa mpito Ndaw na waziri Ouane walipelekwa na wanajeshi hadi kambi ya kijeshi ya Kati karibu na mji mkuu, Bamako.
Hali ambayo ilizua wasi wasi wa kutokea kwa mapinduzi ya pili ndani ya mwaka mmoja nchini humo huku waziri wa Ulinzi Souleymane Doucouré pia ameripotiwa kuzuiliwa.
Ripoti ya kuzuiliwa kwa viongozi hao ilikujua saa kadhaa baada ya serikali kufanya mabadiliko ambayo yalipelekea kuondolewa kwa maafisa wawili wa ngazi ya juu jeshini waliohusika katika mapinduzi ya mwaka jana.
Kwa mara nyingine tena Mali inakabiliwa na hali ya msukosuko miezi ndani ya tisa tu baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’oa madarakani Rais Ibrahim Boubakar Keïta