26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Mabaki ya mwili wa Mugabe kufukuliwa

Harare, Zimbabwe

Mabaki ya mwili wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe yatarajiwa kufukuliwa na kuzikwa upya katika makaburi ya kitaifa kufuatiwa agizo la kiongozi wa kitamaduni nchini humo.

Mugabe alifariki mwaka 2019 na alizikwa nyumbani kwake Kutama kulingana na ombi lake na wala sio katika makaburi ya mashujaa wa kitaifa katika mji mkuu Harare.

Familia imesema Mugabe alikuwa ameelezea hofu yake kwamba mahasimu wake wa kisiasa waliomuondoa madarakani mwaka 2017 huenda wakatumia mabaki yake kufanya kafara ikiwa atazikwa katika makaburi ya kitaifa.

Siku ya Jumatatu, chifu wa kitamaduni katika wilaya ya Zvimba, magharibi mwa mji mkuu wa Harare, alisema kwamba amepokea malalamishi kutoka kwa jamaa wa ukoo wa Mugabe kuhusu mahali alipozikwa.

Pia kiongozi huyo aliamua kuwa Grace Mugabe alikuwa na makosa kwa kukiuka muongozo wa kimila kwa kumzika mume wake nyumbani kwake.

Hata hivyo mke wa Mugabe hakufika mbele ya mahakama ya kitamaduni kusikiliza kikao hicho, lakini chifu alimpiga faini ya kulipa ng’ombe watano na mbuzi mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles