24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Uganda yapata Spika mpya wa Bunge

Kampala, Uganda

Bunge la Uganda limemteua Jacob Oulanyah ambaye ni mbuge wa Jimbo la Kaunti ya Omoro Kaskazini mwa nchi hiyo kuwa Spika wa Bunge la 11 kwa ushindi wa jumla ya kura 310.

Mbuge Oulanyah amechukua nafasi ya Rebecca Kadaga, aliyekuwa Spika wa kwanza mwanamke nchini humo, ambaye alishikilia wadhifa huo kwa miaka 10 pia alikuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 30.

Pia katika kinyang’anyiro hicho cha kutafuta Spika kilisababisha mvutano ndani ya chama tawala cha NRM, huku wakosoaji wa Kadaga wakisema ameshikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu.

Wikendi iliyopita, chama hicho kilimuidhinisha Oulanyah, ambaye alikuwa naibu wa Kadaga kuwa mgombea wake katika kinyang’anyiro cha Uspika.

Kufuatia uchaguzi wa mwezi Januari, Uganda sasa ina bunge kubwa zaidi la wajumbe 529.

Wabunge pia watamchagua naibu wa Spika katika kikao chao cha kwanza ambacho kilifanyika katika Uwanja wa Uhuru wa Kololo, ili kudhibiti maambukizi ya corona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles