30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ulega asisitiza ukuaji wa sekta ya maziwa nchini

Na EDWARD KINDELA – Tanga

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Abdallah Ulega amesema fursa mbalimbali zinazojitokeza mkoani hapa zitasasaidia kukuza sekta ya maziwa.

Aliyasema hayo jana akiwa katika ziara ya siku moja mkoani hapa.

Katika ziara yake, alikutana na Mkuu wa Mkoa, Martine Shigella na kuzungumza na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU).

Mara baada ya kufika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ulega alipokea taarifa ya mkoa iliyoainisha changamoto zilizopo katika sekta ya mifugo na uvuvi mkoani hapa.

Katika taarifa hiyo, Shigella ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuzidi kutoa elimu kuhusu operesheni mbalimbali ambazo zinafanywa na wizara hiyo ili kuondoa usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza kwa wananchi, hususani wanaofanya shughuli za uvuvi katika mwambao wa Bahari ya Hindi.

Pia alimfahamisha Naibu Waziri Ulega ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Rwanda kuwa ni fursa kubwa ya kuwezesha uzalishaji wa maziwa katika Mkoa wa Tanga kupitia matumizi ya bandari na ubia wa kiwanda cha Tanga Fresh, hivyo wizara haina budi kuwawezesha wafugaji kupata ng’ombe wa kisasa ili kuzalisha maziwa kwa wingi na kufaidika na ushirikiano huo.

Akibainisha hatua mbalimbali za Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuboresha sekta ya maziwa, Ulega alisema fursa mbalimbali zinazojitokeza mkoani hapa ikiwemo ujumbe kutoka Rwanda kutumia bandari ya Tanga na kuweka ubia na kiwanda cha Tanga Fresh kutasaidia kukuza sekta ya maziwa.

Katika hatua nyingine, akizungumza na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU), Ulega alibainisha kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Dawati la Sekta Binafsi imeiuanganisha Benki ya Kilimo (TADB) na TDCU kutoa mikopo ya ng’ombe takribani 300 kwa wafugaji mkoani hapa ili kukuza uzalishaji wa maziwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles