29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge awataka vijana kuchangamkia fursa

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

VIJANA nchini wameaswa kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwamo namna bora ya kuanzisha vikundi ili kuomba fedha za halmashauri ambazo zimekuwa zikikosa waombaji katika maeneo mengi.

Imeelezwa kuwa sababu kubwa fedha hizo zinazotolewa maalumu ili kuwakomboa vijana kiuchumi kukosa waombaji ni uelewa mdogo juu ya upatikanaji wake.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Katimba (CCM), katika kongamano la vijana aliloandaa kwa kushirikiana na taasisi yake ya Wezesha, akishirikiana na Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (TES), ikikutanisha viongozi wa makundi mbalimbali jijini hapa.

Akizumgumzia changamoto hizo, Katimba alisema wapo watu wanaoamini kuwa fedha hizo hazipo au zinatoka kwa watu maalumu bila kujua kwamba hazitoki mtu mmoja mmoja.

Alisema kinachotakiwa ni kuungana katika makundi na kuainisha vipengele vya kimkakati, jambo ambalo limekuwa halifanyiki.

“Mimi nawakilisha vijana kule bungeni, lakini pia tunaelekea kwenye bajeti mpya, hivyo naamini pamoja na mambo mengine, tukitoka kwenye kongamano hili la kuwezesha, kuelimishana sambamba na kufungua milango ya kuiona fursa, naamini tutakuwa katika nafasi nzuri, zaidi uwezo wa vijana kuzichangamkia pia fedha za Serikali katika halmashauri zetu,” alisema Katimba.

Akizumgumzia kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa FES, Andreas Quasten, alimpongeza Mbunge Zainabu kwakuwa karibu na vijana akisema anawawakilisha vizuri bungeni.

Katika kongamano hilo la siku moja, vijana mbalimbali walichambua changamoto wanazokutana nazo mitaani, bila kusahau mwelekeo unaoatakiwa kufuatwa katika bajeti kuu ya Serikali itakayosomwa baadaye mwaka huu bungeni jijini Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles