23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ulaya wamwaga neema Ludewa

DEO Na Mwandishi Wetu, Ludewa
NCHI za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) zimetoa Sh bilioni 11.3 kwa ajili ya kusaidia kupeleka umeme kwa wananchi 50,000 wa vijiji 20 vya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe .
Rais wa Shirika lisilo la kiserikali la ACRACCS la Italia, Nicola Morganti, alikuwa akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo ambao ulifanyika katika Kijiji cha Lugarawa jana.
Alisema mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Kanisa Katoliki Dayosisi ya Njombe na Serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
“ACRACCS kupitia Dayosisi ya Njombe waliandika andiko la mradi na kupeleka EU ambao ndiyo wametoa fedha kufadhili mradi huu.
“Jina la mradi ni umeme wa maji kwa vijiji 20 vilivyojitenga wilayani Ludewa na mradi huu umeanza tangu Septemba mwaka 2014 hadi August 2018,” alisema Morganti.
Mwakilishi wa balozi wa EU nchini, Filiberto Cerian, alipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inayoonyesha kwa EU hasa katika kuendesha miradi hiyo ya umeme.
Akizungumzia mradi huo, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), alisema umefika wakati mwafaka kwa wananchi kunufaika na mradi huo ambao utabadili maisha ya wananchi na kaya 4400 zitanufaika zikiwamo shule za msingi na sekondari 43, hospitali na zahanati.
“Tumeupokea mradi huu kwa mikono miwili tunaomba wafadhili muendelee kutusaidia ili vijiji vyote viwe na umeme kwa vile mradi huu ni mkubwa na utasaidia sana uchumi wa wilaya yetu kuimarika na maisha ya wananchi wetu kubadilika.
“Ninawapongeza EU , UNIDO, REA kwa kukubali kufadhili mradi huu ambao utasaidia kuboresha huduma ya umeme katika Wilaya yetu ya Ludewa ikizingatiwa miaka minne iliyopita ni vijiji vitatu pekee kati ya 77 vya wilaya yetu ndivyo vilikuwa na umeme, ila kwa sasa tuna vijiji 67 vina umeme na vimebaki vijiji 10 ambavyo bado havina umeme,” alisema Filikunjombe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles