24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

ULAJI WA PILIPILI HUWASAIDIA WATU WANENE

pilipili-2

Na HERIETH FAUSTINE,

PILIPILI ni tunda kama yalivyo matunda mengine ambalo linavunwa katika mmea ama mche mdogo unaobeba pilipili kama maua.

Zipo aina mbalimbali za pilipili, moja ya aina hizo ni pilipili hoho, mbuzi, mauwa, nyanya, paprika, manga na pilipili kichaa.

Watu wengi wamezoea kutumia pilipili kwa ajili ya kuongeza ladha katika chakula bila ya kujua kama tunda hilo lina faida nyingi katika mwili wa binadamu endapo litatumika kwa ufasaha.

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la American Journal of Clinic Nutririon, limethibitisha kuwa pilipili husaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.

Jarida hilo linasema ulaji wa pilipili unaweza kuwasaidia watu wanene (overweight) au wanaougua ugonjwa wa kisukari kusawazisha sukari kwenye damu.

Pia pilipili ina aina mbalimbali za vitamin ikiwemo A, C na K ambazo zina umuhimu mkubwa katika mwili wa binadamu.

Tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa vitamini A iliyopo katika pilipili husaidia kulinda mwili usishambuliwe na magonjwa kama ya moyo na saratani

Vilevile tunda la pilipili husaidia kuweka sawa kiwango cha joto mwilini kutokana na kuwapo kwa kemikali iitwayo Capsaicin ambayo ndio inayosababisha muwasho.

Pilipili huleta hamu ya kunywa maji na kuondoa mafuta mwilini kutokana na kuwa na muwasho.

Pilipili inasaidia kuweka uwiano wa mzunguko wa damu kutoka katika moyo kwenda sehemu zingine za mwili.

Pilipili husaidia kupunguza cholesterol na kupunguza kiasi cha fibre katika damu.

Pia husaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic kwa asilimia 23 katika muda wa saa tatu hivyo kuchoma mafuta yaliyopo katika mwili.

Husaidia kupunguza maaumivu na uvimbe kwenye tezi na pia kuwasaidia wagonjwa wa uvimbe wa mifupa ya kwenye jointi kupata nafuu.

Aidha tunda la pilipili huzuia kutokwa damu katika kidonda kilichotokana na kujikata. Vilevile huzuia fangasi na bakteria kuingia katika uwazi wa kidonda husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles