28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Ukawa wavamia nyumbani kwa Rais Kikwete

duniNa Elias Msuya, Bagamoyo

MGOMBEA Mwenza wa Chadema kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Juma Duni Haji, ametinga wilayani Bagamoyo na msafara wake ikiwa ni mwendelezo wa safari zake za kampeni.

Wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo, makada wa umoja huo, waliwataka wananchi wa Bagamoyo kumchagua mgombea urais, Edward Lowassa, ili atatue kero zao.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Zanzibar), Ali Said Mohamed, alisema wilaya hiyo ndiko anakotoka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Rais Jakaya Kikwete na Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhwani Kikwete, lakini maendeleo yake hayafanani na viongozi hao.

“Leo hii shule ya mwisho kwa umasikini ipo wilayani Bagamoyo. Miaka 51 ya uhuru Bagamoyo haina maji safi, sisi kule Pemba tuliikataa CCM, leo tunapata maji baridi ya kunywa,” alisema.

Naye Duni alisema umasikini uliopo Tanzania umeletwa na CCM, hivyo akawataka wananchi kufanya mabadiliko kwa kukiangusha chama hicho kupitia sanduku la kura.

“CCM inatuharibia jamii inayokuja miaka 50 ijayo, ndiyo maana tunataka mapinduzi. Hatuahidi kufanya kila kitu, lakini tutajenga vyuo vya ufundi stadi ili vijana wapate ajira. Tunataka kwenda Ikulu ili kina mama wapate matibabu mazuri.

“Rais Kikwete alisema atawanunulieni bajaji, mmezipata? Kina mama hawataki bajaji, wanataka huduma bora za afya ili watoto wazaliwe walete maendeleo,” alisema Duni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles