30.4 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Stars kwanza, lazimawakae

TAIFA1Nigeria football teamNA MELCKZEDECK SIMON, DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo inacheza na Nigeria ‘Super Eagles’ katika kusaka tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika 2017 (Afcon), zitakazofanyika nchini Gabon.

Stars ambayo kwa mara ya mwisho ilishiriki michuano hiyo mwaka 1980, iliyofanyika mjini Lagos, Nigeria, inasaka nafasi ya kushiriki tena michuano hiyo.

Timu hiyo inaanzia nyumbani katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Watanzania wakiwa na matumaini ya Stars kufanya vizuri kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

Taifa Stars inayonolewa na kocha wa muda, Charles Boniface Mkwassa, ilikuwa ikisuasua hapo mwanzo ilipokuwa chini ya kocha Martin Ignatus ‘Mart Nooij’.

Mkwassa alirithi mikoba ya kuinoa Stars baada ya kutimuliwa kwa Nooij, ambaye rekodi yake haikuridhisha.

Nooij alisitishiwa mkataba wake baada ya Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Uganda katika michuano ya kuwania kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi ya Ndani ya nchi zao (CHAN), uliochezwa Julai mwaka huu, kwenye Uwanja wa Amaan mjini  Zanzibar.

Taifa Stars iko kwenye kundi G pamoja na Chad, Misrina Nigeria ambapo Tanzania inashika nafasi ya 140 katika viwango vya ubora vilivyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), vilivyotolewa Julai mwaka huu na imeendelea kushikilia nafasi hiyo kwa mwezi Agosti.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkwassa alisema wamejipanga kwa nguvu zote na watahakikisha wanapata ushindi, ingawa mchezo unatarajiwa kuwa mgumu.

Alisema anamatumaini makubwa ya kushinda baada ya kutengeneza kombinesheni nzuri ya washambuliaji; John Bocco, Mrisho Ngassa na Mbwana Samatta ambaye anacheza soka ya kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Alisema pamoja na Samatta kupata maumivu kidogo katika mazoezi yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini kwa ujumla kikosi chake kiko tayari kwaajili ya vita.

“Tutaingia kwanguvu na kutengeneza nafasi za kufunga kadiri ya uwezo wetu ili kupata bao la mapema ambalo litawachanganya wapinzani wetu,” alisema Mkwassa.

Mkwassa anajivunia makipa, Ally Mustafa, Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Kelvin Yondani, Hassan Isihaka na nahodha, Nadri Haroub ‘Cannavaro’.

Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Salum Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva na Farid Musa, huku safu ya ushambuliaji ikiwa na John Bocco, Rashid Mandawa, Ibrahim Ajib, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa na Mbwana Samatta.

Waamuzi watakaochezesha mchezo huo wanatoka nchini Rwanda ambao ni Louis Hakizima na (mwamuzi wa kati), Honore Simba (mwamuzi msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (mwamuzi msaidizi), AbdoulKarim Twagiramukiza (mwamuzi wa akiba) wote kutoka Rwanda na kamisaa ni Charles Kasembe kutoka nchini Uganda.

Stars inahitajikufanyavizurinakuwekarekodinyinginekatikamichuanohiimikubwabaraniAfrika, hilolinawezekana.

Kama kikosi kile kilichoshiriki fainali zile nchini Nigeria mwaka 1980, waliweza ni imani ya kila Mtanzania pia hata kikosi hiki kitaweza.

Kikubwa ni wachezaji kuweka mbele uzalendo, kujituma na kucheza kwa bidii kuhakikisha tunaifunga Nigeria na kuwa chachu ya kufuzu kw afainali hizo.

Watanzania wanahitaji kuona Stars ikifuzu tena kwa mara ya pili katika fainali hizo za Afcon.

 

Rekodi yaTaifa Stars dhidi ya Nigeria

 

Septemba 11, 2002,   Tanzania 0 Nigeria 2,mechi ya kirafiki.

Desemba 20, 1980, Tanzania 0 Nigeria 2 mechi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Desemba 6, 1980, Tanzania 1 Nigeria 1 mechi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Machi 8, 1980 Tanzania 1 Nigeria 3 mechi ya Afcon

Januari 12 1973 Tanzania 1 Nigeria 2 mechi ya All Africa Games.

Julai 6, 1972 Tanzania 0 Nigeria 0 mechi ya kirafiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles