24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ukawa wamvuruga Mrema wa TLP

mremaNa Safina Sarwatt, Moshi

MWENYEKITI wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustine Mrema, amesema mgombea urais wa Ukawa kupitia Chadema, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa hana ubavu wa kushinda katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu.

Alisema mgombea huyo kupitia  Ukawa hawezi kushinda nafasi hiyo kwa kuwa hana uzoefu na siasa za upinzani na ni CCM “B”.

Mrema aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa kampeni ya mgombea urais wa TLP, Maximillan Lyimo, iliyofanyika katika viwanja vya njia panda ya mji mdogo wa Himo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mrema ambaye aliwahi kugombea urais   mwaka 1995 kupitia chama cha NCCR Mageuzi, alisema anashangazwa na maneno yanayoenezwa na Ukawa kwamba yeye ni CCM wakati wao wamemchukua mgombea wa urais kutoka chama hicho tawala.

“Ukawa wanaita mimi CCM B’wananichafua kwa wananchi wangu na kama
mimi ni CCM mbona nimekaa upinzani kwa zaidi ya miaka 20 na mgombea
wao aliyetoka CCM hajakaa hata mwezi  aitweje? Basi na mgombea wao ni
CCM” B’,”alisema Mrema.

Hata hivyo Mrema alieleza sababu za yeye kutoungana na vyama hivyo vinne vinavyounda Ukawa  akisema umoja huo hauna msaada wowote kwa wananchi bali ni wa maslahi ya mtu mmoja na chama chake.

Pia Mrema alitumia mkutano huo kuiponda Chadema kwamba siyo ile ya zamani bali imetekwa na CCM.

“Niwaambie kwamba mimi ni mpizani wa kweli ndiyo maana nimebaki na
chama changu sijaburuzwa na mtu, tuna msimamo leo hii ningekuwa mgeni wa
nani kama ningejiunga na Ukawa ninyi wenyewe ni mashahidi maprofesa
wamekimbia,  yuko wapi Dk. Slaa?” aliuliza Mrema.

Naye Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mrikario,aliwataka wanawake  kutokudanganywa na baadhi ya wanasiasa wasiokuwa na nia njema kwa kuwarubuni na kuwahonga vitenge na fulana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles