28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ukawa, CCM mambo mazito

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, akiongoazana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, January Makamba (kushoto), nje ya Hotel ya Sea Cliff wanapofanya kikao pamoja na wajumbe wa Ukawa. Picha ndogo ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akiwahi katika kikao hicho jijini Dar es Salaam jana. Picha na Fidelis Felix.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, akiongoazana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, January Makamba (kushoto), nje ya Hotel ya Sea Cliff wanapofanya kikao pamoja na wajumbe wa Ukawa. Picha ndogo ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akiwahi katika kikao hicho jijini Dar es Salaam jana. Picha na Fidelis Felix.

Na Patricia Kimelemeta

KIKAO cha kutafuta maridhiano kuhusu mchakato wa Katiba mpya kilichofanyika jana baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kiligubikwa na usiri mkubwa.

Kikao hicho kimefanyika zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kuanza tena kwa Bunge maalumu la Katiba Agosti 5, ambapo Ukawa bado wanashikilia msimamo wao wa kutorejea bungeni.

Kikao hicho kinachofanyika chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi mwendelezo wa kikao cha awali kilichofanyika Juni 26, mwaka huu ambacho kilishirikisha makundi hayo mawili.

Kikao hicho cha siri kilianza jana saa nne asubuhi katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Masaki, jijini Dar es Salaam, ambapo pande mbili zimekuwa zikivutana kuhusiana na misimamo yao.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kuwa, wajumbe wa pande zote mbili wanadaiwa kulishana yamini kutovujisha siri za kikao hicho kilichotawaliwa na usiri.

Jaji Mutungi aliingilia kati suala hilo baada ya kuona mwafaka wa Ukawa kurudi bungeni umekwama, kutokana na madai ya wajumbe wa CCM kujadili kudaiwa kujadili mambo yasiyokuwamo ndani ya Rasimu ya Katiba.

Madai mengine ya Ukawa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kutumia madaraka yake vibaya ikiwa ni pamoja na kupindisha kanuni za Bunge hilo.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Mutungi alilazimika kuwaita viongozi wa CCM na Ukawa ili kutafuta maridhiano ikiwa ni pamoja na kuwataka Ukawa kurudi bungeni.

Hali ilivyokuwa jana

Kikao cha jana kilifanyika katika usiri mkubwa na habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho, zilisema kulikuwa na mvutano mkubwa miongoni mwa wajumbe waliohudhuria kikao hicho.

Hata hivyo, baadhi ya wajumbe waliobahatika kuhojiwa juu ya mwenendo wa kikao hicho walisema wao si wasemaji na kueleza kuwa msemaji ni Jaji Mutungi.

“Tumekubaliana kuwa msemaji ni mmoja tu, naye ni Msajili wa Vyama, hivyo siwezi kuzungumza lolote kama mnataka taarifa mtafuteni yeye,” alisema Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

Naye, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotoka nje ya ukumbi na kuulizwa kuhusu taarifa za kikao alijibu kwa kusisitiza kuwa yeye si msemaji.

Kinana alisema, taarifa zote zinazohusu kikao hicho zinatolewa na Jaji Mutungi baada, huku akielekea kupanda gari lake na kuondoka.

Kutokana na hali hiyo, waandishi walilazimika kuweka kambi katika hoteli hiyo kwa siku nzima ili kujua kilichojiri katika kikao hicho.

Hadi tunakwenda mitamboni usiku jana hapakuwapo na taarifa rasmi kuhusu maazimio ya kikao hicho na hatima ya Ukawa kurudi bungeni au laa.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. JAMANI MIMI NINAOMBA SANA HIZI PANDE ZINAZOVUTANA ZISIKAE CHINI NA KUANGALIA NINI CHA KUFANYA ILIKUENDELEA NA MJADALA HUU.

    KWA MAONI YANGU NINGEOMBA HAWA NDUGU ZETU CCM WAJARIBU KUKUBALIANA NA KUIFUATA RASIMU ILIOKO MEZANI HALAFU WAJE WAWASHAWISHI WANANCHI KATIKA UPIGAJI KURA WAIKATAE KIPENGELE CHA SERIKALI TATU KAMA JINSI WAO WANVYOONA INAFAA.
    \KATIKA MTAZAMO WANGU MIMI NINAVYOONA NI KWAMBA WENZETU WA ZANZIBAR WANACHODAI NI MAMLAKA KAMILI KATIKA SERIKALI YAO SASA IKIWA HIVYO KIUKWELI HAYAWEZI KUPATIKANA KWA KUWA NA SERIKALI MBILI AU MOJA MAANA UNAPOSEMA SERIKALI MBILI MAANA YAKE TUTAKUWA NA SERIKALI YA ZANZ NA ILE YA JAMHURI KAMA ILIVYOKUWAPO TANGU HAPO AWALI.

    USHAURI WANGU: KWA SASA WANANCHI WAMEBADILIKA SANA INASHAURIWA SERIKALI NAYO ILIJUE HILO, WANANCHI WA ZANZIBAR WANATAKA MAMLAKA KAMILI. PIA UKITEMBELEA ZANAZIBAR WANANCHI WENGI WA HUKO WANAAMINI ZANZIBAR IKIPATA MAMLAKA KAMILI ITAPATA MAENDELEO MAKUBWA, HIYO NDIO IMANI YAO SASA SIO RAHISI WAKUELEWE IKIZINGATIWA SASA HIVI KUNAZO CHANGAMOTO ZA AINA NYINGI MOJAWAPO NI ILE YA AJIRA.

    KWANINI TUANAOGOPA SERIKALI TATU?

  2. KINACHOTAKIWA NI KATIBA YA WATANZANIA SI KATIBA YA CHAMA FULANI NA SI KATIBA YA KIKUNDI AU MTU FULANI KWA MASLAHI YAKE AU MASLAHI YA WAO BINAFSI. NA MCHAKATO HUU UMLIANZA VIZURI KWA KUWASHIRIKISHA WANANCHI KUTOA MAONI YAO. KINACHOKWAMISHA NI NINI KAMA SI MATAKWA YA KUNDI LA WATU AU MATAKWA YA MTU? NAWASHAURI WENYE DHAMANA YA KUIKAMILISHA KATIBA YA WATANZANIA WAKAE CHINI WATUPATIE KATIBA YETU YENYE UHAI ENDELEVU WA TANZANIA NA RASILIMALI ZAKE.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles