29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ukata wakwamisha safari ya wabunge SADC

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WABUNGE wamedhihirisha serikalini kuna ukata wa fedha kutokana na miongoni mwao kushindwa kuhudhuria vikao vyote vya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akizungumzia hali hiyo mjini Dodoma jana, alisema ukwasi umefikia hatua ya wabunge kushindwa kuhudhuria vikao muhimu vya SADC, jambo ambalo linasababisha Tanzania kukosa mambo muhimu.

Alisema ukosefu wa fedha umesababisha safari ambazo ni za muhimu kwa wabunge kuhudhuria nje ya nchi kuzuiliwa, akitolea mfano mikutano ya SADC.

“Hata muda wa shughuli za Bunge umefupishwa, ukiangalia katika hali ya kawaida huwa tunajadili Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa siku tano, Bunge hili jambo zito kama hili linajadiliwa kwa siku tatu, tunajaribu kuhoji kulikoni kumbe hakuna fedha,” alisema Mbowe.

Suala la ukata lilijitokeza kwa mara nyingine kwa wabunge mwanzoni mwa wiki hii, walipokutana katika kikao elekezi.

Katika kikao hicho, bila kujali tofauti zao za itikadi za kisiasa, wabunge waliitolea macho Serikali wakitaka kufahamu hatima ya wananchi ‘kufungishwa mikanda’ kwa lazima.

Wabunge hao waliieleza Serikali kuwa wamechoshwa na vilio vya wananchi vinavyotokana na ukosefu wa fedha.

Mmoja wa wabunge waliohudhuria kikao hicho, alisema: “Tulizungumzia mengi, kila mtu bila kujali wadhifa wake, suala la taasisi na hata mihimili ya Bunge kutokuwa na fedha lilitawala kikao chetu, tulishikamana dhidi ya Serikali tukitaka hali hii itafutiwe ufumbuzi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles