33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

UJERUMANI YALAANI MPANGO WA NYUKILIA WA MAREKANI

BERLIN, UJERUMANI


WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Sigmar Gabriel, ameungana na Urusi, Iran na China, kulaani mipango ya Serikali ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuboresha na kuongeza kiwango cha silaha za nyuklia.

Gabriel alisema umefika wakati Umoja wa Ulaya (EU) kuongoza shinikizo la kuwapo dunia isiyo na silaha za nyuklia.

Kauli hiyo ameitoa kujibu tathmini ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani kuhusu kitisho cha nyuklia katika miongo ijayo.

Mpango huo uliotangazwa Ijumaa iliyopita, unaainisha wazi mkakati mpya wa utawala wa Trump wa kijeshi na nyuklia.

Wizara hiyo ya ulinzi pia imezitaja Urusi na China kama kitisho kikubwa kinachoikabili Marekani.

Silaha za nyuklia za Marekani kwa miongo kadhaa zimewagawa wanasiasa wa Ujerumani.

Wakati Ujerumani yenyewe haina mpango wake wa nyuklia, Marekani imeendelea kuhifadhi vichwa 20 vya makombora ya nyuklia na idadi kubwa ya wanajeshi kwenye ardhi ya Ujerumani tangu mwishoni mwa vita vikuu ya pili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles