27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ujenzi stendi mpya Mbezi wafikia pazuri

Tunu Nassor -Dar es salaam

UJENZI wa Stendi mpya ya mabasi ya kwenda mikoani na nje ya nchi iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaaam imefikia asilimia 60.

Akizungumza katika ziara iliyofanywa na Bodi ya Bodi ya Usajili wa wabunifu Majengo na wakadiriaji Majenzi katika eneo hilo, Meneja mradi huo, Yasin Mringo alisema muda uliobaki wa miezi sita unatosha kukamilisha.

Alisema nyingi zilizokuwa zinakwamisha ujenzi huo sasa zimetatuliwa na nyingine zinaendelea kujadiliwa na Serikali.

“Mradi umefikia asilimia 60 na tunatarajia kumaliza kwa wakati kama yalivyo makubaliano katika mkataba,” alisema Mringo.

Alisema ili serikali kupata faida katika mradi huo inatakiwa kuhakikisha eneo linalozunguka mradi linapimwa na kupangiwa matumizi.

“Eneo linalozuunguka mradi halijapimwa na ni makazi holela hivyo ni vyema kwa serikali kulipima na kupanga matumizi yake kuelekeza wapi kutakuwa na hoteli na huduma nyingine zinazoendana na stendi hii,” alisema Mringo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Ludigija Bulamile aliishauri serikali kuweka wazi miradi inayotaka kuitekeleza ili wananchi ambao ni wanufaika wa miradi hiyo waweze kutoa maoni yao.

Alisema bodi hiyo imekuwa ikipeleka wataalamu wake kujifunza katika miradi mikubwa ili baadaye kupunguza idadi ya wataalamu wanaokuja kusimamia mirahi hiyo.

“Tumekuja kujifunza hapa na kujua namna wataalamu wetu tuliowaleta wanashiriki kikamilifu katika miradi hii,” alisema Dk Bulamile. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles