Mwandishi Wetu, Ukara
Hatua ya kukiinua na kukinusuru kivuko cha Mv Nyerere kilichozama wiki iliyopita kisiwani Ukerewe, umekamilika kwa asilimia 85.
Aidha, Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema jeshi limekamilisha kazi ya kukiinua kivuko na kwamba atakabidhiwa taarifa yake kwa ajili ya wizara yake kuifanyia kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, amesema kazi ya kukinyanyua majini baada ya kuzama kivuko cha Nyerere imekamilika kwa asilimia 85 na baada ya kukamilisha hatua hiyo kwa sasa kazi itakayofanyika ni tathimini na kukivuta kuja ufukoni kwa ajili ya matengenezo kazi ambayo itabaki mikononi mwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).
Hata hivyo alitoa shukrani kwa vikosi mbalimbali vya ulinzi wakiwemo Jeshi la Polisi Maji, Jeshi la Akiba (mgambo), Zimamoto na Uokoaji, wazamiaji pamoja na kampuni za Songoro Marine, Kamanga Ferry, Mkombozi Fisheries pamoja na mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kutoa vifaa.