25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Uhusiano kati ya kitambi na ulaji wa kupindukia

vs2NI dhahili kuwa kila mtu nikimwambia  anipe tafsiri ya neno ‘njaa’ atanipa. Na kwa tafsiri ambayo imezoeleka njaa ni ile hali ya kukaa muda mrefu bila kupata chakula chochote.
Basi baada ya kufahamu hilo, sasa leo nataka uniambie wewe hali ambayo huwa inakukumba ni kweli njaa au ni hali nyingine?

  1. Njaa pia ni tafsiri ikiwa ina maanisha unahitaji chakula.
    2. Njaa ni tafsiri kuwa muda wa kula umefika.
    3. Njaa ni tafsiri kuwa umekaa muda mrefu bila kula ‘nina njaa kali kweli’ kama ni rafiki yako utamuuliza, mbona unakula kwa pupa hivyo? Atakwambia nina njaa mno akimaanisha amekaa muda mrefu bila kula.
    4. Njaa inaweza kuletwa na kitu kitamu na chenye harufu nzuri kimepita karibu, utashtukia unachomoa fedha kwenye pochi na kuchukua chochote.
    5. Njaa pia ni tafsiri kuwa unajisikia angalau kupata chochote tu, kwa sababu tu ule muda rasmi wa kula umepita. Basi utaagiza soda, keki na maandazi.

Hizo zote ni tafsiri za neno ‘njaa’ kiuhalisia.

Je, ni kweli unapojisikia yote hayo lazima ule?
Hapana! Tena hili ndilo kaburi la wengi ambalo linazika afya zao. Unatakiwa ujue njia za kujua je, hii ni njaa ya aina gani? Si kwa sababu machinga kapitisha keki basi kuna hali fulani ya kutaka kula inakuja mpaka unanua unabugia basi moyo unaridhika. Unatembea njiani umechelewa nyumbani eti tu kwa sababu saa sita imepita unaanza kujenga mazingira ya njaa inayotokana na mazoea, hapo ikipita soda unanunua ili tu ukonge moyo wako kuwa angalau umepata chochote.
Umefika kwa rafiki yako, umekuta kakaangiza pilau inanukia kweli, hapo hapo utaaanza kujihisi kutaka kula kwa sababu chakula kinanukia vizuri. Nini tafsiri ya mifano yangu?
Si kila njaa ina maanisha unatakiwa kula, jifunze kutambua chanzo cha kukufanya ujisikie kutaka kula, ukijua hilo utakuwa umeepuka njaa zenye kuepukika naziita “false hunger.”

 

UKITAKA KUPUNGUA UZITO ONGEZA IDADI YA MILO HASA KIFUNGUA KINYWA

Nimekuwa nikifundisha watu lishe salama kiafya na jinsi ya kupunguza uzito kiafya bila ya kuhangaika kabisa huku ukiwa unabaki kuwa mwenye nguvu za kutosha. Neno ‘Breakfast’ silipendi sana maana watu wengi hawalitumii kama linavyo maanisha katika uhalisia wa afya.

Neno Break fast linaundwa na maneno mawili ambayo ni ‘Break’ na ‘Fast’ kwa pamoja neno hili linamaanisha ulikuwa katika mfungo hivyo unasitisha mfungo wako, lazima upate chakula chepesi kwanza kabla ya mlo mkubwa kama vile kuchangamsha mfumo wa chakula kwa sababu ulikuwa umepunguza kasi ya utendaji wakati wa mfungo. Ndio maana Waswali wakasema; “Kifungua kinywa”… ina maana ulikuwa umefunga kwa saa kadhaa sasa unafungua mfungo wako.
Kufunga kupo kwa aina nyingi, unaweza kufunga kwa maelekezo ya daktari wako au unaweza kufunga kiimani. Mfungo wa kiafya unaweza ukawa saa 8,12,16,20,24,36 n.k na hata kile kitendo cha kula usiku saa moja ukaenda kulala hayo hizo ni saa za mfungo, ingawaje mfungo wa usiku huwa si mkali kama wa mchana.

Itaendelea wiki ijayo…

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles