27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Uhuru apiga marufuku samaki kutoka China

NAIROBI, KENYA

WAFANYABIASHARA wa samaki nchini hapa wamefurahi baada ya Rais Uhuru Kenyatta kupiga marufuku kuagiza samaki kutoka nje hususan  China.

Amri hiyo iliyotangazwa juzi ilitolewa baada ya wafanyabiashara wa hapa kulalamika kuwapo ushindani mkubwa sokoni.

Rais Kenyatta alitoa uamuzi huo  aliposhiriki majadiliano kuhusu masuala ya wafanyabiashara wadogo katika Chuo Kikuu cha Biashara cha Strathmore mjini hapa.

Juni mwaka huu wavuvi kutoka eneo la Ziwa Naivasha walilalamika kuwa samaki wa kigeni wamejaa sokoni jambo linalowakwamisha.

Mwaka 2016, Gavana wa zamani wa Kisumu, Jack Ranguma aliitaka Serikali Kuu kupiga marufuku   kuagiza samaki kutoka China kwa sababu hilo linakwamisha biashara.

Hata hivyo, Shirika la Taifa la Viwango Kenya (KBS) lina mtazamo tofauti.

Tathmini ya mwaka 2018 ya KBS, inatahadharisha kuwa Wakenya watasubiri muda mrefu zaidi kabla ya kuona tofauti kwa vile  samaki wanaovuliwa nchini hapa hawatoshi.

Takwimu zinaonyesha idadi ya samaki imekuwa ikipungua kwa   miaka mitatu mfululizo kutokea tani 98,000 mwaka 2016 hadi tani 92,000 mwaka uliopita katika Ziwa Viktoria.

Hilo limesababishwa na magugu maji yaliyoenea na mbinu zisofaa za uvuvi kadhalika idadi ya   sangara kupungua.

Hali kama hiyo imeonekana Ziwa Turkana, ambako idadi ya samaki waliovuliwa wamepungua kutokea tani 70,000 mwaka 2016 hadi tani 4,000 mwaka jana.

Chanzo cha hali hiyo ni mbinu zisofaa za uvuvi na kuhifadhi samaki pamoja na maji ya Ziwa Turkana kukauka.

Lakini pia katika Bahari ya Hindi, idadi ya samaki na viumbe wengine vinavyoliwa imepungua kwa asilimia 3.7 kutoka tani 24,000 mwaka 2016 hadi tani 23,000 ya sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles