24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

UHURU AKOSOLEWA KWA KUWAPONGEZA POLISI

NAIROBI, KENYA


RAIS Uhuru Kenyatta amekosolewa kwa kitendo chake cha kuwashukuru maofisa wa polisi kwa kazi waliyotekeleza wakati wa uchaguzi uliokamilika hivi karibuni ingawa ripoti nyingi zimewashutumu kuua raia wasio na hatia.

Alitoa pongezi hizo katika barua ya siri ambayo ilisambazwa kwa makamanda wa kaunti mbalimbali Ijumaa iliyopita.

Lakini muungano wa upinzani wa NASA, ulisema kwa kushukuru polisi, Rais Kenyatta alithibitisha kuwa anawajibika kwa mauaji waliyotekeleza.

“Kwa kukiri hadharani kuwa polisi wamekuwa wakiua watu kisheria, Uhuru amethibitisha polisi hawakwenda kinyume na maagizo yake.

“Kwa hivyo, anawajibikia na uhalifu ambao polisi waliagizwa kutekeleza. Amejihakikishia nafasi yake kizimbani katika mahakama za Kenya akiondoka madarakani,” ilisema NASA kwenye taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Salim Lone ambaye ni mshauri wa kinara wa muungano huo, Raila Odinga.

Aidha mmoja wa maofisa wa shirika la kiraia la Civil Society Reference Group (CSRG), Suba Churchil, alisema kwa kuwapongeza polisi wanaolaumiwa kutumia nguvu kupita kiasi na kuua Wakenya wasio na hatia, Rais Kenyatta alionyesha kuwa anaunga mkono vitendo vyao.

Kwa mujibu wa Churchil, kwa kuwapongeza maofisa hao, Rais Kenyatta alithibitisha polisi walioua watu walikuwa wakitekeleza sera ya Serikali.

“Nchi yote inasikitika kuwa Rais anaweza kuwapongeza maofisa wa polisi wakati familia za waliouawa na maofisa hao kwa kutekeleza haki zao za kuandamana, zinapoendelea kuchukua miili ya wapendwa wao kwenda kuizika.

“Matokeo ya hali hii yatakuwa ni ukatili zaidi, ukiukaji wa haki za binadamu na kuepuka adhabu kwa maofisa wa polisi, ambao kaulimbiu yao siku hizi si “utumishi kwa wote” bali kulinda masilahi ya Serikali iliyo madarakani,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles