24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Uhai wanyamapori Mikumi, shakani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Ajali za barabarani si tu zina gharimu uhai wa wanadamu la hasha! hata uhai wa Wanyamapori nao uko mashakani kutokana na ajali za barabarani, ambapo inaelezwa kuwa katika hifadhi ya Taifa Mikumi wanyama 700 kila mwaka wanapoteza uhai kwa kugongwa na magari ambayo yanapita katika hifadhi hiyo.

Kiasi cha kilomita 50 za hifadhi hiyo zimepitiwa na barabara kuu ya Morogoro -Iringa ambayo wakati wote inatumika na magari makubwa na madogo.

Kupita kwa magari hayo mahali hapo, kumekuwa kukisababisha vifo kwa wanyama wanaovuka barabara kutafuta mahitaji mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maji na chakula, kutokana na kugongwa.

Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), sambamba na baadhi ya wahariri walifika katika hifadhi hiyo na kujionea hali halisi, ambapo Afisa Mwanadamizi na Mkuu wa Kitengo cha Utalii, Herman Mtei amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kunusuri uhai wa Wanyamapori ambao amesema ni tumu ya taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles